TAARIFA KUHUSU MABADILIKO MADOGO KATIKA MUUNDO WA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA

calendar_monthSeptember 16, 2026 TAARIFA KWA UMMA

16/09/2026

TAARIFA KWA UMMA

MABADILIKO MADOGO YA MUUNDO WA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA

Baraza la Mitihani la Zanzibar linapenda kuwajulisha walimu, wanafunzi, wazazi/walezi na wadau wa elimu kuwa limefanya mabadiliko madogo katika muundo wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba. Mabadiliko hayo yamefanywa kwa lengo la kuhakikisha kuwa Mtihani wa Darasa la Saba unaenda sambamba na matakwa ya Mtaala wa Elimu ya Msingi uliotolewa na Taasisi ya Elimu Zanzibar mwaka 2022.

Aidha Muundo huo unapatikana sasa katika tovuti ya Baraza la Mitihani la Zanzibar (Publications> Miundo ya Mitihani).

 

Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR

north